Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa Manispaa Mtwara-Mikindani, Mwalimu Hassan Nyange amesema Uchaguzi Mkuu ujao utakaofanyika Oktoba usiwe kigezo cha kutugawa wananchi badala yake tuzingatie amani na umoja wa kitaifa.
Mwalimu Nyange ameyasema hayo leo tarehe 11 Mei, 2025 wakati wa kikao na Wadau wa Siasa wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kilichohusu Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili.
Alisema ni vema tukadumisha umoja na amani tulionayo kwani hata Muheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan anasisitiza hilo kupitia falsafa ya 4R (Maridhiano, Ustahimilivu, Mageuzi na Kujenga upya) hivyo basi wananchi tuungane, tupendane na na tuthaminiane ili kudumisha amani iliyopo.
Aidha aliagiza wadau hao kuwasisitiza wananchi juu ya umuhimu wa kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la Wapiga kura ili wapate haki yao kikatiba kwani kura moja tu inaweza kuleta mabadiliko makubwa.
Awali akimkaribisha Mkurugenzi, Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mtwara Mjini, George Mbogo alisema lengo la kikao hicho ni kupeana maelekezo kwa vyama vya siasa kuhusu Uboreshaji kwa Daftari la kudumu la Wapiga Kura unaotarajia kuanza tarehe 16 Mei, 2025 hadi 22 Mei, 2025.
Naye Afisa Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini, Bi. Mwanahamisi Chimbende alisema wadau wanalo jukumu kuwaeleza wananchi kujitokeza kuboresha taarifa zao kwa wale waliojiandikisha awali na wamehama Kata au Jimbo moja kwenda jingine, Waliopoteza sifa mfano wale waliofariki kuondolewa katika Daftari, Wenye taarifa zilizokosewa wakati wa uandikishaji, Pamoja na wale Waliopoteza au kadi zao kuharibika.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.