Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile amewasisitiza Madiwani na watalaamu kuelekeza nguvu katika ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya ndani ili zipatikane fedha zitakazosaidia kutatua changamoto za wananchi ikiwemo ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amesema kuwa katuka kipindinhiki cha msimu wa korosho kila mtu akijitoa kwa nafasi yake katika kufanya kazi ya ukusanyaji mapato tutakwenda kupunguza ama kumaliza changamoto zilizopo.
Hayo ameyasema Leo Novemba 8,2924 kweye Mkutano wa Balaza la Madiwani robo ya Kwanza kwa ajili ya kupitia taarifa za Halmashauri uliofanyika katika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha Ndile amewasisitiza viongozi waliohudhuria mkutano huo kuendelea kupaza sauti katika kuwahimiza wananchi kushiriki kupiga kura ifikapo Novemba 27,2024kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Mstahiki Meya ametumia mkutano huo kuwakaribisha wajumbe pamoja na viongozi mbalimbali kushiriki katika Uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu “Uchaguzi Ndile Cup" Novemba 9,2024 katika uwanja wa Titanic uliopo Kata ya magengeni kwa ajili ya kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupira kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.