Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara -Mikindani Mhe.Shadida Ndile amesema kuwa Manispaa itaendelea kuyaishi maono ya Mhe. Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha inakuza Utalii kwa kulinda na kutunza vivutio vilivyopo ili vizazi vijavyo viweze Kurithi na kuenzi tamaduni za Kitanzania.
Ameyasema hayo Leo Desemba 7,2024 Mchinga -Lindi alipohudhuria kwenye Uzinduzi wa Tamasha la "Tendaguru Mjusi Festival" baada ya kumaliza bonanza la Michezo lililowashirikisha Madiwani wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani na Madiwani wa Manispaa ya Lindi.
Aidha Mstahiki Meya amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Kwa kuwakaribisha na amewapongeza Kwa kuendesha Tamasha la "Tendaguru Mjusi Festival" lenye lengo la kuvutia Utalii Mkoani Lindi.
Aidha amewakaribisha Madiwani wa Manispaa ya Lindi kutembela Manispaa ya Mtwara-Mikindani ili kuendeleza ujirani mwema pamoja kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo Mji Mkongwe wa Mikindani.
Katika Uzinduzi huo uliofanyika Eneo la Mchinga waheshimiwa Madiwani na Wataalamu walitembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika eneo hilo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.