Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele amewataka wadau wa Uchaguzi Mkoani Mtwara kutumia majukwaa mbalimbali katika kuwahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye zoezi la Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga Kura litakaloanza Januari 28 na kumalizika Februari 3 mwaka huu.
“ Ufanikishaji wa zoezi hili utategemea na mchango wa wadau katika kutoa elimu, ni matumaini yetu kuwa mtakuwa wadau wazuri wa kuhamasisha zoezi la Uboreshaji ili watu wajitokeze kuboresha taarifa zao” amesema Mhe. Mwambegele
Ameyasema hayo Leo Januari 16,2025 ,Kwenye Mkutano wa Tume na wadau wa Uchaguzi kuhusu zoezi la Uboreshaji wa daftari La kudumu La Wapiga Kura uliofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania uliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani
Aidha Mhe Mwambegele amewasisitiza Mawakala wa Vyama vya siasa kutoingilia Mchakato wa zoezi zima la Uboreshaji wa daftari la kudumu badala yake amewasihi kufuata kanuni na miongozo iliyotolewa na kufanya mawasiliano na Tume pale inapotokea changamoto ili kuwekana sawa.
Ameendelea kutoa rai rai kwa wananchi kujiepusha na kosa la kujiandikisha zaidi ya mara moja huku akiwahimiza wadau waliohudhuria Mkutano huo kutoa ushirikiano Kwa Maafisa watakaoendesha zoezi hilo.
Uboreshaji wa daftari la kudumu la Wapiga unahusisharaia wa Tanzania wenye umri unaoanzia miaka 18 na zaidi na na watakaofikisha u
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.