Wavuvi wa samaki Manispaa ya Mtwara-Mikindani huenda wakapata ahueni ya kutumia nishati mbadala ya taa zinazotumia umeme wa jua badala ya kutumia karabai zinazotumia mafuta ya taa ambayo yana gharama kubwa na pia ni hatarishi kwa viumbe vya baharini.
Wavuvi wanatarajia kupata ahueni hiyo mara baada ya kuwasilisha changamoto walizonazo kwenye uvuvi wa Samaki walipotembelewa na ugeni kutoka Mji wa Pfrozheim-Ujerumani Julai 14,2022 katika soko la Samaki la feri.
Aidha kwa kuwa hadi sasa wavuvi hao wanatumia zana za zamani kwenye uvuvi wa Samaki ikiwemo (matumizi ya mitumbwi), Ukaushaji wa Samaki kwa kutumia jua,ukaangaji wa Samaki kwa kutumia kuni , wavuvi hao wameuomba ugeni huo kuwawezesha kwa kuwapatia vifaa vya kisasa bila gharama ypyote au kwa gharama nafuu ili waweze kuvua kisasa na kuongeza uzalishaji.
Bi. Dorothea Nulstch kiongozi wa msafal wa ugeni huo ameonesha kuguswa na changamoto za wavuvi hao na ameahidi kuyafanyia kazi maombi yao.
Aidha ugeni huo pia umetembelea Bandari ya Mtwara kuona uendeshaji wa bandari hiyo Pamoja na shule ya Sekondari ya Shangani kuona namna shule hiyo inavyotunza mazingira kwa upandaji wa miti.
Shule nyngine iliyotembelewa ni Shule ya Sekondari ya Call Vision kuona matumizi ya nishati mbadala ya umeme unaotumia upepo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.