Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wajane wa mAnispaa ya Mtwara-Mikindani kutikata tamaa baada ya kupoteza wanaume zao badala yake wafanye kazi kwa bidii ili waweze kuziendesha familia zao
Mhe.Kyoba ameongea hayo Juni 24, 2021 alipozungumza na wajane walipoadhimisha siku ya wajane Duaniani iliyofanyika kataika Ukimbi wa Shule ya Sekondari ya Call Vision iliopo Manispaa ya Mtawara –Mikindani.
Amesema kuwa Serikali inatambua uwepo wa wajane hapa nchini na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtawara ya Mtwara Mikindani kuwakusanya wajane hao kwenye vikundi na kuwapatia mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.
Aidha Kyobya amewapongeza wajane hao kwa kujitambua na kuunda umoja wao pamoj na kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanay ya kulea familia zao.
Kwa upande wake……. Amaeishukuru Serikali kwa kuipa uzito siku ya wajane na kuwatambua wajane kwa kuwawezesha mikopo na kuiomba Serikali kuwashirikisha kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.