Baada ya kupokea fedha Shilingi 440,000,000 za ujenzi wa Madarasa ishirini na mbili ya Shule za Sekondari NANE zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya Oktoba 28,2021 amezindua Mkakati wa ujenzi wa madarasa hayo kwa kuchimba Msingi katika Shule ya Sekondari ya Bandari kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Manispaa, Bodi za Shule, walimu pamoja na wananchi.
Katika Uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya amezitaka shule zote zilziopata fedha za ujenzi kuhakikisha wanajenga madarasa hayo ndani ya wiki nane huku akiwaasa wananchi kushiriki kikamilifu katika kuchangia nguvu kazi ili madarasa yaweze kukamilika kwa wakati.
Amezitaka bodi za shule kusimamia vizuri ujenzi huku akisisitiza kutumia mafunzi wenyeji (force account) katika ujenzi huo na amewataka Mkurugenzi na Mstahiki Meya kuwa na mikakati mizuri ya kuhakikisha wanafunzi hawakai chini.
Pamoja na Shule ya Bandari ambayo imepokea fedha Tsh. 80,000,000 za ujenzi wa madarasa manne, shule zingine zilizopokea fedha ni Pamoja na Shule ya Sekondari Chuno madarasa manne (Tsh. 80,000,000), Shule ya Sekondari Shangani madarasa manne (Tsh. 80,000,000).
Shule zingine ni Pamoja na Shule ya Sekondari Mitengo madarasa mawili (Tsh. 40,000,000), Shule ya Sekondari Naliendele madarasa mawili (Tsh. 40,000,000), Shule ya Sekondari Mtwara-Ufundi madarasa mawili (Tsh. 40,000,000) , Shule ya Sekondari ya Sino Tanzania Friend Ship madarasa mawili (Tsh. 40,000,000)Pamoja na Shule ya Senkondari Mangamba madarasa mawili (Tsh. 40,000,000).
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.