Ikiwa imebaki siku moja ili zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la Orodha ya wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa limalizike hapa nchini , Vijana wa Tarafa ya Mikindani ambao bado hawajajiandikisha wametakiwa kujiandikisha ili waweze kuwa wapiga kura halali na kuchagua kiongozi bora atakaewaletea Maendeleo kwa ajili ya kesho yao iliyo bora.
Aidha wametakiwa kufanya michakato yote ya Uchaguzi kwa kuzingatia amani, utulivu na mshikamano kwa watu wote na kutokubali kutumiwa na mtu au chama chochote kuleta vurugu kwenye uchaguzi huo.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara COL. Patrick Sawala alipozungumza na vijana hao Leo Oktoba 19,2024 kwenye kikao kilichoandaliwa na Diwani wa Kata ya Mtonya Mhe. Shadida Ndile kilichokenga kuwahamasowha Vijana Kujiandikisha na Kupiga Kura Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Kuelekea zoezi la Uchukuaji wa fomu za kugombea nafasi ya Mwenyekiti na ujumbe wa Serikali ya Mtaa kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba 1, Mkuu wa Mkoa amesema kuwa anatamani kuona vijana wengi wanajitokeza kugombea nafasi hizo hivyo amewataka wajitathmini ili muda wa kuchukua fomu ukifika wakachukue na wagombee nafasi mbalimbali.
Ameendelea kuwasisitiza vijana hao kujitokeza kusikiliza sera za wagombee muda wa Kampeni ukifika ili Novemba 27,2024 wakapige kura kuchagua kiongozi mwenye maadili, mtiifu atakayewaletea Maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya yaMtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya amempongeza Diwani wa Mtonya kwa kuwakusanya vijana hao pamoja kwa lengo la kuwapa hamasa ya kujiandikisha na amewataka vijana kutomuangusha na kuwasisitiza wajitokeze kujiandikisha kwa wingi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.