VIJANA NA WANAWAKE MTWARA-MIKINDANI WAPOKEA MILIONI 154.1
Katika kutekeleza agizo la Serikali lililotaka halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake na vijana Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani imeendelea kuneemesha vikundi vya wajasiriamali hao kwa kuwapatia mkopo wa shilingi milioni 154,180,000 kwa awamu ya kwanza.
Mkopo huo uliotolewa kwa vikundi 48 vya wanawake na Vijana kupitia mfuko wa Wananwake naVijana(WDF) umelenga kuwasaidia wajasiriamali hao kukuza mitaji yao ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi mfano wa hundi kwa wanavikundi hao iliyofanyika kwenye ukumbi wa boma mkoa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mh.Evod Mmanda amewataka wanavikundi kutumia mkopo waliopewa kwa weledi na maarifa ya kutosha.
Amesema kuwa ili mkopo uwe na tija kwenye familia zao ni lazima wanavikundi hao waangalie shughuli wanazozifanya na kutafakari kama shughuli hizo zinafaida kiuchumi au la ili waweze kutafuta shughuli mbadala.
Pia amewaasa wanavikundi hao kutotumia mkopo nje ya malengo kwani kutumika nje ya malengo inaletwa taswira ya kuwa wanavikundi hao hawakujipanga na watashindwa kurejesha kwa wakati hali itakayopelekea watu wengine fursa ya kupata mikopo.
MManda amesema kuwa wakati Tanzania ikielekea kwenye viwanda wajasiriamalia mali hao wajipange kwa ajili ya kupata ajira kwa wageni watakaokuja kujenga viwanda lakini ni fursa kwao kwakutengeza bidhaa nzuri kama nguo, kupika chakula kwa mama lishe na uzoaji wa taka zinazozalishwa. Aidha amewataka waboreshe huduma zao ili waweze kupata fursa zaidi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa Bi Beatrice Dominic amesema kuwa Manispaa kwa sasa inaangalia vikundi vya akina mama ambao tayari wapo kwenye viwanda vidogo ili iwatafutie eneo na kuwaweka pamoja kwa ajili ya kuuza bidhaa zao. Hivyo amewataka wajipange kw a ajili ya kuingia kwenye aina nyingine ya ujasiriamali ya viwanda vidogovidogo.
Nae chilumba mwakilishi wa vijana ameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwajali na na kwamba atahamasisha viana wengine ili waweze kujiunga kwenyevikundi na kupatiwa mikopo lakini amewataka wajasiriamal wengine waliopewa mikopokurejesha fedha kwa wakati.
Awali akisoma taarifa ya Mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya Jamii Juliana Manyama alisema kuwa Vikundi vilivyoomba mkopo vilikuwa 88 vyenye jumla shilingi 453,000,000 lakini baada ya uchambuzi vikundi vilivyokidhi vigezo ni 78 vyenye jumla ya shilingi 291,684,300. Hata hivyo mkopo uliotolewa wa shilngi milioni ni 154,180,000 ni awamu ya kwanza kwa vikundi 48 vikiwemo vya wanawake 40 na vijana 8 na kufanya wanufaika wa mkopo huo kuwa 240.
Kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Manispaa imetenga Shilingi milioni 487,514,286 kwa ajili ya mfuko wa Wanawake na Vijana(WDF) ambayo ni sawa na Asilimia 10 ya mapato ya ndani na itanufaisha vikundi 110.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.