Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Abdalah Mwaipaya ametoa rai kwa Vijana kutumia fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo kutumia mitandao ya Kijamii kujinufaisha kiuchumi.
DC Mwaipaya ameyasema hayo kwenye Kongamano la Uwezeshaji Vijana Kiuchumi na Fursa 'KIJANA TIMIZA NDOTO YAKO' lililofanyika katika Ukumbi wa Polisi Mess uliopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani na kuhudhuriwa na vijana zaidi ya 1000.
"Unaitumiaje mitandao ya Kijamii, inakunufaisha vipi, kuna watu wako very strategic wanaingia pesa nyingi kupitia mitandao... Tusifuate tu umbea huko, tuitumie kwa manufaa," alisema DC Mwaipaya.
Alisema ni vyema Vijana wakaacha kujibweteka badala yake wajishughulishe kwenye shughuli mbalimbali zitakazowajenga na kuwapa nguvu ya kiuchumi ili wapete kuheshimika.
Aidha, alitumia jukwaa hilo kuwasisitiza Vijana kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao huku wakiendelea kudumisha Amani na Utulivu.
Kongamano hilo limekuja na Kaulimbiu: "Kijana kwa Maendeleo ya Uchumi, Mtaa Kwa Mtaa"
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.