Vijana wapatao 60 kutoka kwenye Kata tano zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani Agosti 10,2023 Wamepatiwa mafunzo ya kutambua fursa mbalimbali za kujiajiri na kujitolea kushiriki shughuli za kijamii kwenye maeneo yao.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi Juliana Manyama amesema kuwa mafunzo wanayowapa vijana hao itawasaidia kuzikimbilia fursa zilizopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Amesema kuwa ili kuwafikia vijana wengi zaidi Manispaa itajitahidi kutafuta wadau wengine iliwaweze kufadhili mafunzo kama hayo katika Kata zilizobaki.
Akizungumza kwa naiba ya vijana wenzake Derick Musiba ameishukuru Manispaa na MSOPAO kwa kuandaa mafunzo hayo kwani yatawasaidia vijana kwenye kuchangamkia fursa ili waweze kujiajiri.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mnaispaaa ya Mtwara-mikindani kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la kupambana na umaskini Mtwara (MSOAPO) yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa mikutano wa SIDO Mtwara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.