Mratibu wa huduma ndogo za fedha Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Janeth Mhegele amesema kuwa walimu wa vikoba na vikundi vyote vinavyotoa huduma ndogo za fedha vitakavyoshindwa kujisajili hadi kufikia April 20 mwaka huu vitapigwa faini inayoanzia shilingi Milioni moja hadi milioni kumi.
Pamoja na faini hiyo vikundi hivyo pia vinaweza kupata adhabu nyingine ya kifungo kinachoanzia miezi mitatu hadi miaka miwili jela au adhabu zote mbili kwa Pamoja.
Mhegele amefanunua kuw adhabu hizo zinatolewa kupitia sheria ya fedha ya mwaka 2018 inayotaka vikundi vyote vya kijamii (vikoba na upatu) na walimu wanaofundisha Vikundi hivyo kujisajili hadi kufikia April 30 mwaka huu.
Amebainisha kuwa usajili huo utafanyika bure kwa vikundi vya kijamii lakini kwa walimu (Promoters) watalipia ada ya usajili ya shilingi elfu ishirini.
Usajili wa vikundi hivyo unafanyaika Ofisi za Maendeleo ya jamii huku usajili wa walimu unafanyika katika Ofisi za Afisa biashara zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Zoezi la usajili wa vikundi limeanza April 1 mwaka huu na linatarajia kukamilika ifikapo April 30, 2021.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.