Mkuu wa Wilaya ya Mtwara ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka Viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuhakikisha wanasimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuifanya kuwa ajenda ya kudumu.
Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya amewasisitiza wananchi wa Manispaa hii kila mtu kuwa balozi wa Mtwara kwa kuzungumza mazuri ya Mtwara na kila kitu kizuri kinachofanyika kwenye eneo lake ili Mtwara iweze kukua Zaidi.
Mhe. Mkuu wa Wialaya ameyasema hayo April 29,2022 kwenye IFTAR iliyoandaliwa na Ofisi yake na Ofisi ya Mstahiki meya iliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani , Diwani wa Kata ya Mitengo Mhe. Ibrahim Mnyetuka amewashukuru wananchi wote waliohudhuria kwenye iftari hii na kuwasisitiza kuendelea kudumisha mshikamano huu hata baada ya mwezi wa ramadhani kuisha.
Aidha amewataka kuendeleza utamaduni wa kutemebleana na kushirikiana kwenye mambo mbalimbali ili Manispaa yetu iweze kusonga mbele
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.