Kutokana na kuwepo kwa baadhi ya vitendo vinavyotia aibu na kuathiri ukuaji wa mtoto ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan kyobya amewataka viongozi kuhakikisha kunakuwa na mkakati mahsusi wa kubainisha vitendo hivyo ili viongozi waweze kutatua chnagamoto hizo.
Mhe. Mkuu wa Wilaya ametoa magzio hayo Juni 15, 2022 kwenye sherehe za mtoto wa Afrika zilziofanyika kwa nagazi ya halamshauri katika Viwanja vya Mashujaa.
Aidha amewaasa wazazi kutowatumia watoto kama kitega uchumi kwa kuwacheza ngoma ili mzazi apate nguo na fedha na kumuagiza Kamanda wa Polisi Wilaya ya Mtwara kwa kushirikiana na Afisa utamaduni kuhakikisha hawatoi vibali vya sherehe zenye viashiria hivyo.
Mkuu wa Wilaya pia amewataka watoto hao kutoa taarifa mapema pale wanapoona kuna hataroi ya kufanyika ukatili.
Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani amesema kuwa wao kama viongozi watafuatailia kwa ukaribu na kuhakikisha changamoto zote zinazowagusa watoto wanazisimamia na kuzitatua ili watimize malengo yao.
Akizungumza kwa naiaba ya watoto wenzake Dhauli Juma ameiomba Serikali iandae vitengo maalumu ambavyo watoto Serikali iandae vitengo maalumu ambavyo watoto wataenda kutoa hoja zao bila kuchukuliwa picha jongefu na kutumwa mitandaoni kwani itawapelekea watoto hao kuwa na wasiwasi a kutoa matatizo wanayokutana nayo
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.