Viongozi wa vyama vya Siasa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamehimizwa kuzingatia siasa zenye amani na utulivu ili kufanya Uchaguzi wenye tija na kuepuka machafuko.
Wito huo umetolewa leo Oktoba 21, 2024 na Afisa Usajili kutoka Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa - Dodoma, Zablon Nswila, wakati akizungumza na Wenyeviti na Makatibu wa vyama vya siasa wilaya ya Mtwara kwenye mafunzo yaliyotolewa na Ofisi hiyo katika ukumbi wa Manispaa Mtwara-Mikindani.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwakumbushana mambo yaliyokatazwa kwenye sheria ya vyama vya siasa ili kuendeleza amani na utulivu wa nchi na kufanya Uchaguzi wenye tija.
Kwa upande wake, Afisa Usajili toka Ofisi hiyo, Bi. Jacqueline Kombe, alisema mada za msingi zilizojadiliwa katika mafunzo hayo ni pamoja na Haki na Wajibu wa vyama vya siasa, na Wajibu wa wadau wengine wa uchaguzi ili wasiweze kuvuka mipaka ya kiutendaji hasa kwenye kipindi hiki cha mchakato wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.