Waajiriwa wapya thelathini na tisa wa ajira mpya katika kada za afya , Elimu na Utawala Manispaa ya Mtwara – Mikindani wametakiwa kufanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia kanuni na maadili ya Utumishi Umma.
Rai hiyo imetolewa Julai 28,2022 na kaimu Mkurugenzi wa Manispaa bwana Mangula Mayemba kwenye mafunzo ya waajiriwa hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa ofisi Ya Manispaa.
Aidhi Mangula amewapongeza waajiriwa hao kwa kupata nafasi ya kuhudumu ndani ya Manispaa na kuwakaribisha kuendelea kulisukuma gurudumu la Maendeleo kwa kuhudumia jamii ya wanamtwara
Mkuu wa idara ya Utawala na usimamiziwa ukaguzi wa Rasilimali watu Bi. Upendo Haule amewasisitiza waajiriwa hao kuzingatia nidhamu katika kazi hasa uvaaji wa nguo zilizotajwa kwenye waraka wa mavazi , kuwahi kazini na kutoa huduma bila upendeleo.
Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa kupitia mfumo wa ufundishaji wa kielektroniki (MUKI) washiriki wa mafunzo wamefundishwa mada mbalimbali zikiwemo mfumo wa Serikali za Mitaa , wajibu , haki na maswala ya nidhamu Watumishi wa umma , kanuni na maadili ya Utumishi wa Umma.
Mada zingine ni Pamoja na taratibu za kiofisi pamoja na Usimmizi wa Kumbukumbu na Mawasiliano Serikalini, Usimamizi wa utendaji kazi katika Utumishi wa Umma ,huduma kwa Mteja Pamoja na masuala ya kitaaluma na mtambuka.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.