Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Ngazi ya Kata Jimbo la Mtwara Mjini,wamehimizwa kuwaandikisha Wananchi wenye sifa ili waweze kupata haki yao ya kikatiba itakayowawawezesha kushiriki katika kuchagua Viongozi wao.
Hayo yamesemwa Leo Januari 26,2025 na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Mtwara Mjini Ndugu Allen Ndomba wakati akifunga Mafunzo ya siku mbili ya Waandishi wasaidizi na Waendesha vifaa ya Bayometriki yalifanyika Leo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi.
Alibainisha kuwa ni matarajio ya Tume kuwa,mara baada ya zoezi hilo ni kukamilika kwa wapiga kura wataokuwa wamepatiwa kadi na watakuwa ni wapiga kura halali.
Aidha,amewasisitiza umuhimu wa kuzingatia umakini katika kila eneo iwemo utunzaji wa vifaa vyote.
Kwa upande wake Bi.Fausta Mahenge Afisa Sheria Mwandamizi Kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi amewataka waandishi Wasaidizi kuweka kipaumbele katika kuwaandikisha watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wanawake wajawazito,watu wenye ulemavu pamoja na wagonjwa.
Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litaanza Januari 28,2025 na litakamilika Februari 3,Mwaka huu likiwa na kauli mbiu inayosema “Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora”
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.