Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Jimbo la Mtwara Mjini wametakiwa kutumia uzoefu walionao kutimiza majukumu ya uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura pamoja na kuwasaidia wengine ambao hawakuwahi kushiriki zoezi hilo.
Wito huo umetolewa leo 25/01/2025 na Afisa Mwandikishaji Jimbo la Mtwara Mjini, George Mbogo wakati wa Ufunguzi wa Semina ya Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga kura, iliyofanyika Shule ya Sekondari Mtwara Ufundi.
"Nawasihi kutumia uzoefu wenu mlionao kuwasaidia wenzenu ambao hawajawahi kushiriki katika uboreshaji wa Daftari ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu," alisema.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Afisa Uchaguzi Jimbo la Mtwara Mjini, Mwanahamisi Chimbende aliwaasa waandikishaji hao na watunza vifaa kuzingatia weledi na kuvitunza Vifaa hivyo kwandi ndio msingi wa uadilifu.
Alisema semina hiyo inalenga kuwapa elimu ya kutosha itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao hivyo wayazingayie kwani ndio itaoelekea kufanikisha zoezi hilo.
Zoezi la Uboreshaji Daftari la kudumu la Wapiga kura Jimbo la Mtwara Mjini litaanza tarehe 28/01/ hadi tarehe 03/02/2025.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.