Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani, Leo tarehe 26 Februari, 2025 wameendelea na mafunzo kwa vitendo kuhusu mfumo wa Uandikishaji na matumizi ya 'BVR kit'.
Mafunzo hayo yanaendelea ikiwa ni siku ya pili na ya mwisho ya Semina ya Mafunzo ya Uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura inayofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi.
Mafunzo hayo pia yanahusisha namna Bora ya ujazaji wa fomu,kutumia mfumo wa Kuandikishwa Wapiga kura (Voters Registration system -VRS) pamoja na matumizi sahihi ya Vifaa vya Uandikishaji wa Wapiga kura.
Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa upande wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani litaanza tarehe 28 Januari na kutamatika tarehe 03, mwaka huu likiwa na Kauli Mbiu inayosema "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bor
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.