Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Benki ya Dunia Kupitia mradi wa Uboreshaji Miji Tanzania (TACTIC) wamekutana na wadau wa mazingira kutoka Taasisi mbalimbali zilizopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa ajili ya kupitia matokeo ya utafiti wa mikakati ya usimamizi wa takangumu ili kupata maoni ya mwisho yatakayopelekea kuandaa mpango mkakati wa pamoja wa utunzaji wa mazingira na udhibiti takangumu kwenye mji wa Mtwara lengo ni kuweka Mji huu kwenye hali ya usafi wakati wote.
Ikumbukwe kuwa Utafiti wa mikakati ya usimamizi wa takangumu katika Mji wa Mtwara ulianza kufanyika Juni,2022 na Shirika la Open Map Development Tanzania (OMDTZ) na FB Empowerment ambao walifanya utafiti wao kwenye mitaa saba (Shangani, Rahaleo, Tandika, Reli, Vigaeni , Chikongola na Mikindani) ili kubaini maeneo yenye taka na aina ya taka zinazozalishwa.
Aidha baada ya kazi hiyo kukamilika inatarajiwa kuwepo kwa Mkakati Madhubuti na mpango kazi wa utunzaji wa mazingira na udhibiti wa takangumu kwenye Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Mkutano wa wadau wa kukamilisha utafiti wa mikakati ya Usimamaizi wa taka ngumu (Litter Management Strategies) umeanza Leo Julai 27 na utamalizika Julai 28, 2023.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.