Kufiatia agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kututaka kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga , Manispaa ya Mtwara-Mikindani imetekeleza agizo hilo kwa kuwakatia maeneo ya kufanya biashara katika eneo lililotengwa lililopo nyuma ya stendi ya mabasi yaendayo mikoani Chipuputa.
Afisa biashara wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Janeth Mhegele amesema kuwa tangu zoezi la kuwapatia maeneo lilipoanza februari 3,2022 tayari wafanyabaishara 145 wameshapatiwa meneo kati ya wafanyabiashara 325 walioandikishwa wakati wa mchakato wa wali wa kuwabaini ulipofanyika.
Amesema kuwa eneo hilo limechaguliwa na wafanyabiashara wenyewe baada ya Manispaa kuaianisha maeneo mengi hivyo amewataka waanzekufanya biashara kwa wakati.
Ameendelea kubainisha kuwa katika eneo hilo biashara zote zitauzwa isipokuwa bidhaa za sokoni kama vile matunda , mboga mboga pamoja na bidhaa zingine .
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wengine Bi. Mwajuma Issa ameishukuru Serikali kwa kuwapatia maeneo rasmi ya kufanyia baishara na kuomba serikali kuwatengenezea miundombinu rafiki ili waweze kufanya baishara zao kwa furaha na amani.
zoezi la upangaji wa ugawaji wa maeneo kwa wafanyabaishara wadogo limeanza februari 2,2022 na bado linaendelea kwa wafanyabiashara wengine waliobado kupata maeneo ya biashara.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.