Watumishi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wameungana na wafanyakazi wote Duniani kusherehekea siku ya wafanyakazi na wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza kiwango cha mshahaara kwa asilimia 35.1 ambayo ni sawa na shilingi laki tano (500,000) kwa mtumishi anayepokea kima cha chini.
Akizungumza kwenye hafla fupi ya wafanyakazi hao iliyofanyika katika Ukumbi wa Police Mess, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Ndugu Rugembe Maiga amesema kuwa watumishi wameridhishwa na ongezeko hilo na kwamba ni Faraja kwao kuona Rais Samia ametambua jitihada kubwa inayofanya na watumishi katika kuleta Maendeleohapa nchini.
Aidha watumishi hao wamemuomba Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuendelea kuwakutanisha watumishi Pamoja katika matukio mbalimbali ili kupata burudani ,kujenga umoja na ushirikiano kwenye utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Siku ya wafanyakazi Duniani hufanyika kila mwaka ifikapo Mei Mosi, na mwaka huu sherehe hizo Kitaifa zimefanyika Mkoani Singida na Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Aidha Mkoani Mtwara Sherehe hizo zimefanyika katika Wilaya ya Newala na Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Col. Patrick Kenan Sawala.
Kauli Mbiu ya Sherehe ya wafanyakazi Duniani mwaka huu yalikuwa na Kauli Mbiu inayosema “Uchaguzi Mkuu 2025 Utuletee Viongozi Wanaojali Haki na Maslahi ya Wafanyakazi, Sote Tushiriki”.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.