Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brig. Jen Marco Gaguti amewataka watendaji na watoa huduma wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini kuhakikisha wanatoa huduma bora ili kuendana na matarajio ya Serikali na wananchi kwa ujumla.
“Dhamana mliopewa ni kubwa, Serikali imewaamini na kuwapa nafasi kuhudumu katika Hospitali hii, msiwavunje moyo wananchi toeni huduma kwa kuzingatia ubora” Amesema Gaguti
Mhe. Gaguti ametoa rai hiyo Oktoba 1, 2021 wakati wa ziara yake ya kukagua utekelezaji wa agizo la ufunguzi na kuanza kwa huduma katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini.
Wakati huo huo Mhe. Gaguti amewataka wananchi wa Mkoa wa Mtwara kuitumia Hospitali hiyo kama daraja la kukuza uchumi binafsi kwakuwa uwepo wa hospitali hiyo utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika Mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla.
“Tuitumie hospitali hii kama daraja la kufanikiwa, huduma za kijamii zitaongezeka katika maeneo haya hospitali hii itafungua fursa mbalimbali katika Mkoa wetu” Amesema Gaguti
Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani Said Nassoro ameishukuru Serikali kwa ujenzi wa hospitali hiyo kwakuwa hospitali hiyo itaimarisha afya za wananchi pia pato la Manispaa yetu litapanda.
Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Mohamedi Kodi amesema kuwa Hospitali hii imerahisisha upatikanaji wa huduma za kibingwa , kabla wananchi walilazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama kubwa kufuata huduma.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.