Baada ya kukaa takribani siku saba ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani na kuzungukia maeneo mbalimbali , hatimae julai 19,2022 tumeagana na wageni wetu kutoka mji wa Pforzheim- Ujerumani huku wakionesha nia ya kuweka miundombinu ya taa zinazotumia umeme wa jua kwenye mitaa ambayo barabara zake zimekosa taa za barabarani.
Maeneo mengine walioyoonesha nia ni pamoja na ufungaji wa mfumo wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia nishati ya jua katika Kituo cha afya cha Likombe, utoaji wa taa zinazotumia nishati ya jua kwa wavuvi wa Samaki feri Pamoja na uletaji wa kifaa kitakachotumika kuhifadhia Samaki.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Bi. Dorotea Nulstch amemshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwapokea vizuri na kuahidi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuwezesha sekta mbalimbali.
Amesema kuwa yeye Pamoja na timu yake wamefurahi kuwepo Mtwara na wamejifunza mengi na kuhaidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya taasisi hizi mbili.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amewashukuru wageni hao kwa kutembelea Mtwara na kauhidi kuendeleza uraafiki uliopo na amewakaribisha tena kutembelea Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.