Jumla ya wakazi wapatao 1052 wa Mtaa wa Mwera wana uhakika wa kupata maji safi na salama baada ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu. Ismail Ali Ussi kuzindua mradi wa kisima cha maji katika Mtaa huo uliogharimu Shilingi milioni kumi na tatu laki tano arobaini na moja (13,541,000).
Ndugu Ussi amesema kuwa yeye pamoja na timu yake wanafarijika kuona maendeleo makubwa yanayofanywa na Serikali na kumpongeza Mkuu wa Wilaya, Madiwani na Mkurugenzi na timu yake.
Aidha amewataka wannachi wa eneo hilo kuhakikisha wanaitunza miundombinu iliyojengwa kwa kuwa Manispaa imefanya jitihada kubwa ya kuwaletea maji safi na salama
Afisa Mtendaji wa Kata ya Chikongola Bi. Shakila Twahili amesema wazo la kuchimba kisima hicho lilitolewa na wananchi wa mtaa huo kwa kushirikiana na diwani wa Kata hiyo Mhe. Musa Namtema kutokana na wakazi wake kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji.
Ili kutatua changamoto hiyo Mhe. Diwani alichangia shilingi milioni mbili (2,000,000 ), wakazi wa Mtaa huo nao walichangia Shilingi milioni moja laki saba arobaini na moja ( 1,741, 0000 )na kuanza ujenzi wa kisima hiko.
Hata hivyo baada ya fedha hizo kutotimiza lengo lao , Manispaa ya Mtwara-Mikidani ilichangia Shilingi milioni tisa laki nane ( 9,800,000 ) kutoka mapato ya ndani kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kisima hiko.
Aidha amebainiha kuwa pamoja na wananchi wa Mtaa huo kuwa na uhakika wa kupata maji safi na salama mradi huo pia utasaidia kupunguza umbali mrefu wa kutembea kutafuta maji pamoja na kuongezeka kwa muda wa kufanya shughuli za kiuchumi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.