Wakati Serikali ikiendelea kuboresha mazingira wezeshi kwa wakulima kupitia upatikaji wa pembejeo hapa nchini, wakulima wa korosho Manispaa ya Mtwara -Mikindani wanufaika kwa kupokea ruzuku ya pembejeo za kilimo.
Mkuu wa idara ya kilimo,umwagiliaji na ushirika Bw.Mohamed Longoi , amesema Manispaa ya Mtwara-Mikindani imepokea pembejeo mifuko 1812 ya salta , bedmenol lita 297, subatext lita 148 pamoja na duduba lita 3414 ambazo zinaendelea kusambazwa kwa kutumi kusambazwa kwa wakulima kupitia vyama vyao vya Msingi.
“Wananchi tayari wamepokea pembejeo na wameshaanza kuzitumia kwaajili ya kuzuia wadudu na kutibu magonjwa katika zao la korosho, maafisa kilimo wa Kata na Mitaa wanaendelea kusimamia matumizi sahihi ya viwatilifu hivyo”Amesema Longoi
Kutokana na juhudi za Serikali katika kukuza sekta ya kilimo nchini Bw. Longoi ameishukuru Serikali kwa kurahisisha upatikanaji wa pembejeo Mtwara-Mikindani kwani zimefika wakati sahihi wa matumizi na pia imepunguza gharama za manunuzi ya pembejeo kwa wakulima.
Naye Mwenyekiti wa chama cha Msingi Naliendele Bw. Said Jalulu amesema kuwa muitikio wa wakulima ni mkubwa wengi wamejitokeza kuchukua pembejeo, na ameiomba serikali kuwa zoezi hili liwe endelevu kwa manufaa ya wakulima wa Mtwara.
Naye Bi.theresia Mnunduma ambae ni mnufaika wa ruzuku hiyo ameishukuru Serikali kwa kuendela kuboresha mazingira ya uuzaji wa zao la korosho kwa kuondoa tozo ya shil. 110 kwenye kila kilo moja ya korosho waliokuwa wanakatwa hapo awali.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.