Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe. Edward Kapwapwa amewataka wakusanya taarifa kwenye zoezi la uhakiki wa anuani za makazi kuwa waadilifu na wakafanye kazi kulingana na maelekezo ya Serikali ili zoezi hilo likamilike kwa wakati na kwa usahihi.
“Wapo watu wengi wapo nje walitamani kufanya kazi hii na hawakupata, nendeni mkafanye kazi kwa uadilifu na katika misingi ambayo sisi kama Manispaa hatutaharibu zoezi hilo” amesisitiza Naibu Meya.
Naibu Meya ametoa rai hiyo Desemba 10, 2022 alipokuwa anafungua mafunzo ya zoezi la uhakiki wa anuani za makazi yaliyofanyika Shule ya Sekondari ya Mtwara-Ufundi.
Aidha Mhe. Kapwapwa amewapongeza washiriki wa mkutano huo kwa kupata nafasi ya kufanya kazi hiyo na kwamba ana imani wataifanya kwa ufasaha na umakini mkubwa sana.
Kwa upande wake…… kutoka wizara ya Habari, mawasiliano na teknolojia ya Habari ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuendelea kufanya uhakiki hata kabla ya zoezi hili la uhakiki awamu ya nne halijaanza.
Amesema kuwa zoezi anuani za makazi ni gumu na lina changamoto nyingi lakini amewataka wakusanya taarifa kutokata tamaa badala yake waendelee kujituma kwa kuwa waadilifu ili kazi iwe nzuri zaidi.
Mratibu wa zoezi la anuani za makazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani Abeib Mohamedi amesema kuwa hadi kufikia mwezi Mei halmashauri imeweza kufanya zoezi hilo kwa hatua mbalimbali ikiwemo ukusanyaji wa taarifa za anuani za makazi, uwekaji wa miundombinu ya anuani za makazi Pamoja na uwekaji wa vibao vyenye majina ya barabara na kwamba hadi sasa miundombinu ipo na kila nyumba ina namba.
Mafunzo ya uhakiki wa anuani za makazi yamehusisha wakusanya taarifa wa anauani za makazi, watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na wenyeviti wa Mitaa. Zoezi la uhakiki w anuani za makazi limeanza Desemba 11 na litamalizika Desemba 23,2022
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.