Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mwalimu Hassan Nyange amewataka Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na wasaidizi wao kuhakikisha wanaupokea na kuutumia vizuri mfumo mpya wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa masuala ya kifedha (IFT-MIS) ambao utasaidia kupunguza hoja za wakaguzi ndani ya Manispaa.
Mwalimu Nyange ametoa rai hiyo, Leo Mei 2,2025 alipofunga mafunzo ya siku moja ya mfumo huo kwa Wakuu Wa Idara, Vitengo na wasaidizi wao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha Mkurugenzi amewataka wahusika wa mafunzo hayo kujikita kwenye ujibuji wa hoja za wakaguzi ziliizowekwa kwenye mfumo huo kwa wakati na kwamba hategemi idara au kitengo chochote kitakwamisha zoezi hilo.
Mfumo wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa masuala ya kifedha (IFT-MIS) unalenga kurahisisha uwajibikaji wa Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye kujibu hoja , kufuatilia na kuhakikisha hoja zinafungwa kwa wakati.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2025 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani. All rights reserved.