Baada ya Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kuanzisha mfumo wa Kielektroniki wa utoaji na usimamizi wa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, Septemba 28,2022 Wakuu wa Idara na Vitengo Manispaa ya Mtwara-Mikindani wamejengewa uwezo juu ya ufanyaji kazi wa mfumo huo.
Serikali imeanzisha Mfumo huo ili kutatua changamoto zilizokuwa zinajitokeza hapo awali ikiwemo uwepo wa vikundi hewa, kukosekana kwa uwiano wa mgawanyo wa asilimia kumi za mikopo kwa vikundi na walengwa.
Changamoto nyingine ni watu kujiandikisha Zaidi ya kikundi kimoja, changamoto ya marejesho na kukosekana kwa mikakati Madhubuti ya kusimamia urejeshaji wa mikopo pamoja na utata wa usajili wa vikundi na kuwepo kwa vikundi ambavyo namba zake zimejirudia zaidi ya kikundi kimoja.
Aidha mfumo huu unatarajia kuboresha na kurahisisha usajili wa vikundi, kuzingatiwa kwa utengaji wa fedha kulingana na matakwa ya kisheria kwa makundi husika, utoaji wa mikopo kwa kuzingatia kiwango kilichokubalika tu pamoja na kuimarika kwa usimamizi na ufuatiliaji wa marejesho na shughuli za vikundi.
Afisa Maendeleo ya jamii Bi.Juliana Manyama amesema kuwa mfumo huo utakuwa unatumika kuanzia kusajili vikundi hadi kwenye utoaji wa mikopo hiyo.
Aidha ameishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuleta mfumo kwani imerahisisha utendaji kazi wa Idara inayosimamia mikopo hiyo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.