WALENGWA WA KAYA MASKINI WAPONGEZWA KWA KUJIUNGA NA VIKOBA
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Octavian Lyapembile amewapongeza walengwa waliopo kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini kwa uthubutu walioufanya mkubwa wa kuanza kuweka akiba na kukopeshana kwenye vikoba, ingawa changamoto za ukosoefu wa fedha na mafunzo hazijatatuliwa.
Pongezi hizo zimetolewa kwenye kikao cha uendeshaji wa zoezi la ugawaji wa fedha kwa kaya maskini kilichofanyika Juni 31 kwenye viwanja vya Ofisi ya Kata ya Chikongola.
Lyapembile amesema kuwa, ili kaya maskini ziweze kukuza uchumi na kujitegemea ni lazima wajiunge kwenye vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza, ambapo fedha zinazowekwa zitatumika na walengwa kama mitaji ya kuanzisha au kupanua shughuli zao za kiuchumi.
Aidha Lyapembile amewataka walengwa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(TIKA) ilikugharamia huduma za afya kwa kuchangia malipo kabla ya kuugua na kwa gharama nafuu. Amesema kuwa uchangiaji huo kwa kaya ni Tsh. 5000 kwa mwananchi mmoja ambapo anapata matibabu kwa mwaka mzima.
‘Natambua kuwa mpaka sasa Wananchi 949 kutoka kwenye kaya za mpango wamechangia kiasi Tsh. 4,745,000/= bado idadi ni ndogo ukilinganisha na idadi ya walengwa wote jiungeni kwenye mfuko huo.”alisema Oktavian
Nae Mratibu wa Mradi Bi Sylivia Mwanache amesema kuwa wanaendelea kuwahamasisha walengwa kujiunga kwenye vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana, kwa kuwa suala hilo limezaa matunda, kwani wengi wameweza kutumia pesa kuanzisha au kundeleza biashara zao.
Nae bi Zulfa Sadi amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuleta mpango huo na kwamba kikundi chao kinakopeshana na mpaka sasa kikundi kimeweka akiba ya Tsh. 3,000,000/= ambayo wanatumia kukopeshana na kuanzisha miradi ya kikundi kama vile kutengeneza batiki na kukopeshana sabuni.
Wakati huohuo Bi Deo Mtitu msimamizi wa mradi amewataka walengwa kujiunga kwenye mfuko wa afya ya jamii na kwamba jambo hilo ni la lazima kwa kila mlengwa kwa kujikatia yeye mwenyewe pamoja na watu waliopo kwenye kaya yake.
Mradi wa kunusuru kaya Maskini Manispaa Mtwara-Mikindani una jumla ya Kaya 1,328 kutoka katika Mitaa 36 ya awali. Mradi huu ni wa miaka mitatu na ulianza 05 Novemba 2013 na hadi sasa kiasi cha Tsh. Zimelipwa Tsh.718,222,602.00 kwa awamu 20. Aidha mgeni rasmi aligawa kadi za bima ya afya kwa wazee na walengwa waliochangia mfuko huo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.