Baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya Mitihani wa Taifa ya kidato cha nne na cha pili iliofanyika mwaka uliopita na Manispaa ya Mtwara-Mikindani kutokea kwenye kumi bora kitaifa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko ameandaa hafla fupi ya kuwapongeza walimu, shule na wanafunzi waliofanya vizuri.
Hafla hiyo imefanyika februari 12, 2021 katika Ukumbi wa Chuo Cha Ualimu Kawaida ikiambatana na utoaji wa zawadi na kikombe cha ushindi kwa shule zilizofanya vizuri na fedha taslimu kwa walimu na wanafunzi waliofanya vizuri.
Akiongea katika hafla hiyo MKurugenzi wa Manispaa Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa ameamua kuwapongeza walimu na wanafunzi hao ili kutambua juhudi kubwa walizofanya hadi kuifikisha Manispaa katika hatua ya kumi bora kati ya halmashauri 188 zilizofanya Mitihani hiyo.
Amesema kuwa tukio hilo ni zuri kwani inaleta hamasa na chachu ya watu kujituma ili mwaka huu Manispaa iweze kufanya vizuri Zaidi.
Aidha amewataka walimu waliopata zawadi kutobweteka badala yake waendelee kujituma Zaidi , na kwa wasiopota amewataka wachape kazi ili matokeo yajayo na wao wawe washindi
Katika Matokeo hayo Manspaa imeshika nafasi ya kumi Kitaifa katika Mtihani wa taifa wa kumaliza kidato cha nne na nafasi ya tisa Kitaifa katika matokeo ya Mtihani wa taifa wa kidato cha pili.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.