Baada ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani kufanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi uliofanyika Septemba mwaka huu na kushika nafasi ya pili kimkoa kati ya halmashauri tisa zilizopo mkoani Mtwara, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani amewapongeza walimu pamoja na shule zilizofanya vizuri zaidi ya zingine kwa kuwapatia fedha taslimu Pamoja na vyeti ili kuwatia moyo na kutambua kazi kubwa waliyoifanya.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Desemba 2,2021 katika Ukumbi wa Call Vision Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Col. Emanuel Mwaigobeko amesema kuwa ofisi yake inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na walimu katika kuendeleleza taaluma shuleni kulikopelekea ufaulu kuongezeka kwa asilimia sita mwaka huu.
Amesema kuwa pamoja na kutoa pongezi hizo amewataka walimu hao kutobweteka badala yake waongeze juhudi katika ufundishjai namkuimarisha nidhamu shuleni ili matokeo yanayofuata yawe mazuri Zaidi ya mwaka huu.
Kwa upande wake Afisa Elimu Msingi amesema kuwa ongezeko la ufaulu mwaka huu limechangiwa na mikakati mbalimbali kutoka kwenye Idara ikiwemo kutoa mitihani ya wiki, mwezi na mazoezi mengi kwa wanafunzi, kuongeza muda wa kujifunza kwa walimu wa madarasa ya mitihani kwa lengo la kuwapa mazoezi ya kutosha na walimu kupata muda wa kufanya masahihisho, kuwapa walimu stahiki zao pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula cha mchana.
Katika kuhakikisha kuwa ufaulu huo unaongezeka mwaka ujao idara ya elimu wameweka mikakati ifuatayo kuongeza muda wa kujifunza kwa wanafunzi wa darasa la saba, kutoa maelekezo juu ya utuzi wa mitihani Pamoja na kufanya vikao vya tathmini.
Shule zilizofanya vizuri ni Pamoja na
Katika matokeo ya Mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi yaliyotangazwa Oktoba 30 mwaka huu Manispaa ya Mtwara-Mikindani imefaulisha jumla ya wanafunzi 2443 wakiwemo wavulana 1179 (49%) na wasichana 1264 (51%) sawa na asilimia 92.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.