Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kushirikiana na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya ‘Sports Development Aid’ kupitia mradi wa ‘Imporewed Girls Speak Out’ awamu ya tatu, imetoa mafunzo ya mpira wa Kengele (Goalball) kwa Walimu wa michezo na Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi wenye mahitaji maalum ili waweze kushiriki mashindano ya Umitashumta na Umiseta yanayotarajia kuanzahivi karibuni.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi leo Mei 2,2025, Afisa Michezo wa Manispaa Mack Kayombo amesema kuwa mafunzo hayo yamewalenga Wanafunzi wenye uoni hafifu na wenye ulemavu wa ngozi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kupata timu ya mchezo huo katika mashindano hayo.
Naye Meneja wa mradi Empowe Hirls Speak Out Bi. Jackline Mpunjo amesema kuwa kutokana na kundi hilo kusahaulika katika jamii hususani kwenye suala la michezo, Taasisi yao imeona ni vema kuwapa fursa ya mafunzo ili washiriki kwenye mashindano hayo yenye heshima kubwa kitaifa.
Bi. Mpunjo ameongeza kuwa Mchezo huo pia utasaidia kundi hilo kuepukana na tabia hatarishi ikiwemo utoro, Mimba na ndoa za utotoni huku ikisaidia kujenga afya pamoja na kutengeneza fursa ya ajira kwa siku za usoni.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.