Pamoja na Manispaa ya Mtwara-Mikindani kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka jana kwa kushika nafasi ya kwanza kimkoa na kushika nafasi ya pili kimkoa kwenye matokeo ya darasa la saba , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunsta Kyobya ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa matokeo hayo na kusisitiza kuongeza juhudi ili kwenye mitihani ya Taifa ya mwaka huu matokeo yawe mazuri Zaidi .
Ili kufikia malengo hayo amewataka walimu kufanya maandalizi mapema hasa kwa madarasa ya mitihani kuhakikisha hadi kufikia mwezi julai mwaka huu shule zote ziwe zimeshamaliza kufundisha syllabus ili wanafunzi wafanye mazoezi ya kutosha.
Mhe. Kyobya ameyasema hayo Machi 28 ,2022 kwenye sherehe za maadhimisho ya wiki la juma la elimu yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Majengo.
Aidha Mhe. Kyobya amewataka walimu kufanya mitihani ya kushindanisha Shule kwa shule na shule za Serikali na shule binafsi kwa kila robo ili kuhakikisha wanafunzi wanakuwa wamejiandaa vya kutosha na kuwataka wazazi na walezi kuwaunga mkono walimu kwa kuchangia chakula cha wanafunzi shuleni.
Katika kuwapa motisha walimu na wanafunzi ili waendelee kujituma na kufanya vizuri ameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni moja kwa kila mwanafunzi wa kidato cha sita atakaepata daraja la kwanza pointi tatu, mwanafunzi wa kidato cha nne atakaepata daraja la kwanza pointi saba na mwanafunzi atakaeongoza kwa ufaulu darasa la saba katika Mitihani ya Taifa inayotarajia kufanyika mwaka huu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya wazazi shule ya Msingi Shangani Bwana Jacob Shirima amewataka wazazi kuamka kwa kuchangia chakula cha mtoto shuleni ili kumrahisishia kusoma kwa umakini.
Maadhimisho ya wiki ya jula elimu Manispaa ya Mtwara-Mikindani yamehitimishwa leo na tunajiandaa kwa jili ya kilele cha maadhimisho hayo yanayotarajia kufanyika April 2 Wilayani Newala.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.