Walimu wametakiwa kuwa wabunifu katika vipengele vya ufundishaji ili kuwafanya wanafunzi kujenga tabia ya kupenda masomo,hasa masomo ya sayansi ili kuendana na mabadiliko ya kidunia.
Hayo yamesemwa Januari 24, 2023 na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara Mikindani Bi. Upendo Haule Katika hafla ya usainishwaji wa Mikataba ya utendaji kazi baina ya Mafisa elimu wa divisheni ya Sekondari na Afisa Elimu Msingi dhidi ya Maafisa Elimu kata, Walimu wakuu na Wakuu wa shule kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Mtwara Ufundi
Kaimu Mkurugenzi amewataka walimu hao kutumia akili walizonazo kuziongezea ubunifu kwa Watoto wanaowafundisha ili kuwafanya waelewe kirahisi hasa masomo ya sayansi ambayo yanasadikika kuwa ni magumu.
Aidha Haule aliwasisiza walimu hao kutekeleza yale yote yaliyomo kwenye mikataba wanaliyosainishwa na kuwasisitiza walimu kufanya vikao vya mara kwa mara kwa ajili ya kubadilishana ubunifu na kujua changamoto mbalimbali zinazowakabiri wanafunzi.
Aidha kutokana na uwepo wa wimbi kubwa la Watoto kubakwa na kulawitiwa amewasisitiza walimu hao kusititiza suala zima la malezi na maadili kwa wanafunzi kwa wanafunzi na kutoa elimu ya kujitambua.
Nae Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Mtwara Felista Kibiki amewapongeza walimu wote wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kufaulisha vizuri darasa la saba na kuwataka walimu kuendlea kufundisha kwa bidi ili Manispaa iweze kupata matokeo bora Zaidi
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.