Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mikindani Mhe, Dunstan Kyobya amewataka wananchi wa Mtwara kutoa taarifa pindi wanapoona kuna hatari ya uvunjifu wa amani katika Manispaa hii ili kuendelea kudumisha amani na usalama katika kuleta maendeleo ndani Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mhe. Kyoba ametoa rai hiyo tarehe 7 Mei,2021 kwenye iftari aliyoiandaa kwa kushirikiana na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mikindani , Bi. Shadila Ndile iliyofanyika nyumbani kwa Mkuu wa Wilaya.
Alisema kuwa suala la kulinda amani ni la kila mwananchi, hivyo ametoa wito kwa kila mwananchi kuwa mdau namba moja katika kuendelea, kuimarisha na kulinda usalama na amani kwa maendeleo ya Manispaa hii.
“Jana nimetimiza mwaka mmoja tangu nimekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mikindani, ninashukuru kwa ushirikiano mlionionesha katika kipindi chote hicho, niwaombe wananchi wa Mtwara Mikindani tuendelee kushirikiana katika kudumisha amani kwa maendeleo ya Wilaya yetu”
Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi. Shadida Ndile ametoa wito kwa wananchi waliohudhuria katika hafla hii kushirikiana katika kutatua changamoto zinazoikabili Manispaa kwani maendeleo yoyote lazima yaje na changamoto.
Iftari hiyo ilihudhuriwa na wananchi mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini na Kiserikali pamoja na baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.