Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba Mhe.Hemedi Suleimani Abdulla, ametoa rai kw aWatanzania kuendelea kudumisha Muungano ,Amani na Mshikamano ,sambamba na kuwaunga mkono viongoziili Taifa lizidi kupata Maendeleo zaidi.
Ameyasema hayo Aprili 25,2025 wakati w ahotuba yake katika maadhimisho ya miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanziba , yaliyofanyika kikand akatika viwanja vya Sabasaba Mnaispaa ya Mtwara-mikindani na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Mtwara.
Alisema ni ukweli usifichika nchi yetu imepata maendeleo mengi kupitia Muunganowetu ni dhaman ,heshima na Tunu ya Taifa : Shiriki Uchagzui Mkuu wa Mwaka 2025 : hivyo akawataka wanamtwara kuhakikisha wanashirikiana vyema uchaguzi huo kufanya maamuzi sahihi.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Col. Patrick Sawala alisema tangu kuasisiwa kwa Muungano kumekuwa na mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za kisiasa, kiuchumina kijamii na ameendelea kuwa moja ktai ya vielezo vikuu vya Umoja , udugu na Utaifa wetu kama Watanzania na Mkoa wa Mtwara umepata manufaa makubwa ya kimaendeleo kupitia Muungano
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.