Kufuatia zoezi la utoaji wa kingatiba za mabusha , matende na minyoo ya tumbo lililofanyika Manispaa ya Mtwara-Mikindani kuanzia Septemba 24, 2022 hadi Septemba 30, 2022, Wananchi wapatao 122,249 wamepatiwa kinga tiba kati ya wananchi 142,915 waliolengwa sawa na asilimia 85.
Zoezi la utoaji wa kinga tiba lilifanyika Katika Kata zote kumi na nane na Mitaa mia moja kumi na moja ambapo wagawa dawa walipita nyumba kwa nyumba kutoa kinga tiba hizo kwa Watoto wote wenye umri unaoanzia miaka mitano na kwa watu wazima wote isipokuwa wajawaito na wagonjwa walio mahututi.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.