Mkuu wa Wilaya ya Mhe.Dunstan Kyobya ametoa siku tisini kwa wananchi 184 waliofanyiwa urasimishaji katika mtaa wa Machame uliopo Kata ya Mitengo kuhakikisha wanalipia gharama za umiliki wa hati miliki ili waweze kuishi katika maeneo hayo kiuhalali.
“Tunataka kila mwananchi wa Machame awe na hati miliki, hizi ekari 15 ambazo utaratibu wa urasimishaji umefanyika watu wapatao 236 kupata haki zenu , mpaka kufikia septemba 13 orodha niliyopewa inaonesha kwamba watu 31 hati zenu zipo tayari, watu 19 hati zenu zipo kwenye maandalizi, watu wawili wameanza kulipia fedha nusu kwa ajili ya kupata hati na watu 184 hamjamaliza malipo kwa ajili ya kupatiwa hati zenu sasa nataka hili zoezi lifike mwisho”amesema Kyobya
Ameyasema hayo Septemba 13 alipofanya mkutano na wananchi wa Kata ya Mitengo kwa ajili ya kuhamasisha wananchi wa eneo hilo kulipia gharama za umiliki wa hati miliki za viwanja vyao.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa miezi mitatu kwa wananchi wa machame watakaoshindwa kulipia gharama ya urasimishaji na fidia ya utwaaji wa eneo hilo inayopaswa kulipwa kwa Mkurugenzi kiasi cha shilingi lakini mbili na nusu kwa kila mmoja kuwa watanga’anywa maeneo yao na kupatiwa watu wengine.kunyangaywa kwa viwanja kwa wananchi mia mbili thetathini wa eneo hilo watashindwa kukamilisha kulipa gharama ya urasimishaji na fidia ya utwaaji wa eneo la Machame ambayo inapaswa kulipwa kwa Mkurugenzi ambapo kila mwmanachi anatakiwa kulipa shilingi laki mbili na nusu
Kwa uapnde diwani wa Kata ya Mitengo Ibrahim Mnyetuka amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Mtwara kwa msaada mkubwa alioutoa kwa wananchi wa Machame ana amewahamasisha wananchi hao kujitahidi kwa kila hali hali na mali kuhakikihsa wanalipa fedha ya umiliki wa hati miliki
“
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.