Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya ametoa siku saba kwa wananchi wa Mtaa Machame Kata ya Mitengo kuhakikisha wanalipa gharama za urasimishaji na fidia ya eneo la Machame waliovamia ili waweze kupata hati na kumilikishwa eneo hilo.
“Serikali inatambua uhitaji wenu na imeridhia kuwaachia eneo, ila kasi ya ukusanyaji wa fedha bado hairidhishi natoa siku saba kila mwananchi awe amelipa fedha hizo ili zoezi la upimaji lianze” Amesema Mhe. Kyobya
Mhe. Kobya ametoa agizo hilo leo Septemba 24, 2021 katika kikao chake na wananchi wa Mitaa wa Machame kilichofanyika katika Kata ya Mitengo.
Ili kila mwananchi aweze kukamilisha eneo lake Mkuu wa Wilaya amemtaka kila mwananchi wa eneo hilo kulipa kiasi cha shilingi 100,000 kwa ajili ya urasimishaji na shilingi 1500,000 kwaajili ya fidia ya eneo hilo.
Aidha ametoa rai kwa wananchi wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani kuacha utaratibu wa kuvamia maeneo kiholela na kusisistiza kuwa taratibu za kisheria zitachukuliwa kwa yoyote atakayefanya hivyo.
Naye Diwani wa Kata ya Mitengo Bw. Ibrahim Mnyetuka amewataka wananchi hao kukamilisha uchangiaji wa fedha hizo ili Serikali itumie fedha hizo kutafuta eneo jingine mbadala kwa ajili ya ujenzi wa shule.
Bi. Khadija Musa mkazi wa Eneo hilo amesmshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwapatia eneo hilo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.