Mgogoro wa wananchi wa Mangamba uliodumu kwa miaka ishirini na mbili upo mbioni kumalizika baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Mtwara Mjini Mtwara (MTUWASA) kutoa fedha kiasi cha shilingi milioni mia nane kumi na sita, laki saba themanini na sita elfu mia saba sabini na moja (816,786,971) kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi hamsini na moja ambao maeneo yametwaliwa kupisha ujenzi wa eneo la kutibu maji Mangamba.
Akizungumza katika MKutano na wananchi hao uliofanyika Septemba 9,2022 katika eneo la shule ya Msingi Mangamba , Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Dunstan Kyobya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ulipwaji wa fidia kwa wananchi wa eneo hilo.
Mhe, kyobya amesema kuwa wananchi wote waliofanyiwa tathmini wataanza kulipwa fedha zao Septemba 10,2022 kupitia akaunti zao za benki huku akimuagiza Mkurugenzi wa MTUWASA kuhakikisha anakamilisha malipo ya wananchi hao kwa wakati.
Aidha amewapongeza wananchi hao kwa uvumilivu wa miaka yote ambayo walikuwa wanaidai Seriali bila kufanya vurugu na kuwasihi kuendelea na utamaduni huo kwa masuala mengine ili kuijenga Mtwara ya Maendeleo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wananchi hao wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwalipa fidia kwani walishakata tamaa na Baadhi yao nyumba zao zilishaanza kubomoka.
Wananchi hao pia wamemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Mkurugenzi wa MTUWASA kwa kuwatia moyo na kufuatilia jambo hilo kwa ukaribu hatimae jambo hilo limemalizika kwa amani na fedha zao wanaenda kuzipata.
“Tangu mgogoro huu uanze mmekuwa mkituita mara kwa mara kututia moyo na kutuahidi kuwa jambo hili mnalifuatilia,tulidhani mafanya siasa lakini haikuwa hivyo, tumefurahi kwa jambo hili la muda mrefu leo limemalizika, Mungu awabariki sana viongozi wetu”amesema Shakuru Pesambili kwa naiba ya wananchi wa Mangamba.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.