Ili kuwawezesha watumishi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani kkumiliki viwanja kw aajili ya ujenzi wa nyumba ya makazi Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Mtwara-Mikindani ameridhia hoja ya Wajumbe wa baraza la wafanyakazi Manispaa ya Mtwara-Mikindani la kuwapatia watumishi wake viwanja vya makazi kwa mkopo utakaolipwa kidogo kidogo
Pamoja na viwanja Mkurugenzi pia ameridhia kuwanunulia saruji kwa bei nafuu Kutoka Kiwanda cha Dangote kwa watumishi wenye uhitaji wa kujenga kwa kuwa Mnaispaa imeingia Mkataba na Kiwanda hicho na kupata namba ya uwakala ya ununuzi wa saruji kwa jumla.
Akizungumza katika Mkutano wa baraza hilo uliofanyika Novemba 10,2021 katika Ukumbi mdogo wa mikutano wa Shule ya Sekondari ya Mtwara-Ufundi , Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Juliana Manyama amesema kuwa Pamoja na watumishi hao kupatiwa viwanja kwa mkopo watatakiwa kuwa waaminifu na kuvilipia kwa wakati.
“Ipo tabia hapa imejitokeza kuna watumishi wamepewa viwanja eneo la Mtawanya lakini hadi sasa hawajavilipia sasa kwa hivi ambavyo Mkurugenzi ameridhia kuwakopesha basi tuwe waaminifu na tuvilipie kwa wakati”amesema Juliana
Afisa Mipangomiji wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Bi. Mariam Kimolo amesema kuwa kwa sasa Manispaa imepata Mkopo kutoka Seriklai kuu kwa ajili ya kupima na kuendeleza eneo la Mkangala hivyo kazi ikishakamilika watumishi watajullishwa ili waweze kuomba viwanja.
Kuhusu ununuzi wa saruji kiutoka Kiwanda cha dangote Kaimu Mkurugenzi amewasisitiza watumishi kuwa saruji hiyo itanunuliwa kwa watumishi ni kwa ajili ya ujenzi nyumba na sio kufanya biashara kwa kuwa sio malengo ya Manispaa kuuza saruji .
Kwa upande wake Mratibu wa shirikisho la vyama vya wafanya kazi Mkoa wa Mtwara (TUCTA) Bwana. Athumani Kayumba ameipongeza Manispaa ya Mtwara-Mikindani kwa kuwa halmashauri pekee yenye utaratibu wa kufanya Mkutano huu na kumtaka Mkurugenzi kuendelea na utaratibu huu kwani ni sehemu pekee ambayo watumishi wanaweza kuelezea chnagamoto zao, kutoa maoni na hata kupanga mipango mbalimbali.
Huu ni MKutano wa kwanza wa baraz ajipya la Wafanyakazi lililoundwa mwezi februari mwaka hu una linahusisha watumishi kutoka idara zote zilizopo Manispaa Pamoja na viongozi wa Vyama vya wafanayakazi kama vile TALGWU, TUGHE Pamoja na CWT
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.