Wananchi wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani wametakiwa kuzingatia Usafi wa mazingira katika maeneo yao ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko na kuleta muonekano mzuri wa Manispaa hiyo.
Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya Manispaa hiyo, Mhe. Shadida Ndile wakati akihitimisha kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika leo (07/04/2025) katika ukumbi wa Boma uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Alisema ni vyema Watendaji na Wataalamu wa Manispaa hiyo kuendelea kutoa hamasa na kusimamia zoezi la ufanyaji usafi katika kata zote kuwa endelevu ili kuimarisha usafi wa mazingira katika Manispaa hiyo.
Kwa upande wake, Mwakilishi toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, CPA. Norbert Shee, alipongeza Madiwani na wataalamu wa Manispaa kwa kusimamia thamani ya Miradi.
Kikao hicho cha baraza kimefanyika kwa lengo la kupitia taarifa za kata, kikiwa na jumla ya agenda 5.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2025 Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani. All rights reserved.