Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Mhe. Hassan Mtenga amewataka wananchi wa Jimbo la Mtwara Mjini kujenga Imani na viongozi wanaowachagua ili waweze kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo katika sekta mbalimbali.
Amesema kuwa yeye kama mbunge amekuwa akifanya kazi kubwa ya kuhakikisha anaishawishi Serikali ili iweze kuleta miradi ya maendeleo ambapo miradi mingi imetekelezwa na mingine inaendelea kutekelezwa ndani ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Ameendelea kusema kuwa mbunge amefanikiwa kutatua migogoro minne aliyoikuta ikiwemo mgogoro katinya wananci wa California na JWTZ.
Mhe. Mtenga ameyasema hayo Fbruari 29,2024 alipofanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Mtonya kw aajili ya kusikiliza kero zao na kuzipatia majibu.
Mwenyekiti wa UWT Kata ya Mtonya Bi Halima Hamisi amewahamasisha wanawake wa Tarafa ya Mikindani kugombea nafasi ya Uongozi wa Seriklai za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
MKutano huo pia ulihudhuriwa na Naibu Meya wa Manispaa Mhe. Sixmund Lungu pamoja na madiwnai kutoka Kata ya Rahaleo, Likombe na Tandika.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.