Ikiwa zimebaki siku tano zoezi la Uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura likamilike katika Mikoa ya Lindi na Mtwara,Wananchi Mkoani Mtwara wametakiwa kutumia siku zilizobaki kujiandikisha katika daftari hilo.
Wito huo umetolewa Januari 14 na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa alipoenda kurekebisha taarifa zake katika daftari la kudumu la wapiga kura katika kituo cha Shangani Mashariki kilichopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
“Nitoe wito kwa Wananchi wote kutumia siku tano zilizobaki kuhakikisha wanaitumia haki yao ya kimsingi ya kuboresha taarifa zao katika daftari la wapiga Kura ili mwisho wawe na sifa za kugombea na kuchagua, ni haki ya kidemokrasia, ni haki ya kisiasa ni haki ambayo inaenda kuleta mabadiliko kama itatumiwa vizuri katika kujenga na kuleta Maendeleo.”alisema Byakanwa
Aidha Byakanwa ameongeza kuwa kwa taarifa alizozipata zinaonesha kuwa kuna muitikio mkubwa kwa Vijana ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na wale ambao watafikisha miaka kumi na nane ifikapo siku ya Uchaguzi kwamab wamejiandikisha kwa wingi katika kituo cha Shangani Mashariki.
Zoezi la Uandikishaji Wananchi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura limeanza rasmi tarehe 12 Janauari na linatarajia kukamilika tarahe 18 Januari,2020 kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara, Aidha jumla ya Vituo 118 vya kupigia vinaenesha zoezi hilo.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.