Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evod Mmanda amewataka wananchi Wilayani Mtwara kujenga utamaduni wa kupanda miti katika maeneo yao pamoja na kuitunza miti iliyopandwa ili kufanya mazingira kuwa mazuri na yenye kuvutia.
Mmanda ametoa rai hiyo kwenye zoezi la uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika Kimkoa Wilayani Mtwara katika Viwanja vya Shule ya Misngi ya Tandika iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani Februari 14,2020.
Amesema kuwa kumekuwa na takwimu nyingi za upandaji wa Miti lakini changamoto kubwa ni namna gani mapenzi ya kupanda miti yanakwenda sambamba na mapenzi ya kutunza miti..
“Tunaweza kuwa na mapenzi ya kupanda miti lakini mapenzi ya kutunza miti hadi ikakaomaa yasiwepo, tupende kupanda miti,kuitunza miti iliyopo na iliyopandwa” alisema Mmanda
Aidha Mmanda amesema kuwa matumizi ya mkaa yamekuwa makubwa kuliko kasi ya upandaji wa miti na kwamba hali ya ukataji ikiendelea inaweza ikaleta madhara makubwa sana katika utunzaji wa mazingira.
Amewataka wakala wa misitu kanda ya kusini kutoa elimu juu ya sheria za mchakato wa kuvuna mazao ya misitu ili wananchi wawe na uelewa na kuondoa malalamiko pindi wakala hao wanapotekeleza sheria zao.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.