WANANCHI WATAKIWA KUCHUKIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA.
Katika kuhakikisha kuwa Wananchi wa Manispaa Mtwara-Mikindani wanaokoa afya zao kwenye magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa mazingira wametakiwa kuuchukia uharibifu wa mazingira katika maeneo yao.
Hayo yamesemwa jana na Mratibu wa baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira Mkoani Mtwara(NEMC) Bwana Lewis Nzali kwenye maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani, maadhimisho hayo yamefika kwenye viwanja vya mashujaa Manispaa Mtwara-Mikindani.
Nzali alisema kuwa ili tuweze kupiga hatua mbele katika Maendeleo kupitia vipato vyetu, hatuna budi kuweka mazingira katika hali ya usafi kuanzia nyumbani na kila mahali. Aidha amewaomba Wananchi kushirikiana katika kulinda mazingira ili uhusiano wetu na mazingira uzidi kudumu, na mazingira yaweze kuwa mhimili wa viwanda, ambako ndiko Taifa linakoelekea.
Aidha Nazli amewataka wamiliki wa viwanda au shughuli mbalimbali wanatakiwa kuzingatia Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na kanuni zake, kwani kwa kufanya hivyoviwanda havitakuwa chanzo cha afya mbayakutokana na uchafuzi wa mazingira.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara-Mikindani Donald Nssoko amewashukuru wananchi wote pamoja kwa kuendelea kushirkiana na Manispaa katika kuuweka mji katika hali ya usafi na kwamba Halmashauri itaendlea kusimamia sheria za usafi ili mji wetu uendelee kuwa msafi.
Siku ya mazingira hufanyika kila ifikapo 5/6 ya kila mwaka, na mwaka huu Kitaifa imeadhimishwa Butiama ikiwa na kauli mbiu inayosema "Hifadhi Mazingira Mhimili wa Viwanda"
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.