Kutokana na kuwepo kwa janga la Ugonjwa wa CORONA Duniani, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Dunstan Kyobya amewataka wananchi wote Wilayani Mtwara kutochukulia poa Ugonjwa huo badala yake wachukue tahadhari kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wetu wa afya kila mara.
“Tuzingatie ushauri wa wataalum wetu, Nitoe tahadhari juu ya ugonjwa wa CORONA, nawa mikono, vaa barakoa kama hauna ya dukani vaa kitambaa chako au jifunike, tumia vitakasa mikono, tuepuke misongamano isiyo na ulazima, tunapokaa tuache nafasi ili tupeane hewa ya kutosha” Alisema Kyobya
Mhe. Kyobya maetoa rai hiyo Julai,8,2021 alipohudhuria hafla fupiya utoaji wa mikopo ya Vikundi vya Wanawake, Vijana na Wwatu wenye Ulemavu iliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa vilivyopo Manispaa ya Mtwara-Mikindani.
Aidha amewataka Viongozi wa Kata na Mitaa kuendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari huku akiwasisistiza walimu mashuleni, wananchi na wafanyabiashara kuweka kibango cha kunawia mikono, vitakasa mikono pamoja na uvaaji wa barakoa.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.