Katika kuhakikisha Tanzania inaondokona na ukatili dhidi ya wanawake na watoto, Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani Bw. Godlove Miho ametoa rai kwa mwananchi wa Manispaa hii kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kutokomeza ukatili dhidi ya na watoto ili kuboresha ustawi wa mtoto wa sasa na ajae.
"Ukatili huu unafanywa kwenye jamii na unafanywa na wanajamii , hali kwa kweli hairidhishi, jaribu kufikiria hadi sasa tuna kesi 29 zinazohusiana na ukatili wa mtoto, hata mwaka bado haujaisha, nitoe rai kwa wananchi wote tushirikiane kwa pamoja ili tuweze kuondokana na tatizo hili , tusitegemee Serikali pake yake” Alisema Bw.Miho
Miho amesema hayo katika mafunzo ya usalama na ulinzi wa mtoto yanayofanyika Juni 17,2021 katika ukumbi wa shule ya Msingi St. Michael iliyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Miho ameendelea kusisitiza kuwa sio jukumu la Serikali pekee kuhakikisha inatokomeza ukatili dhidi ya watoto bali kila mwananchi ana wito na jukumu wa kuhakikisha anamlinda mtoto dhidi ya ukatili na kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi anapoona viashiria vya ukatili katika jamii inayomzunguka.
Ameendelea kuzitaja aina za ukatili dhidi ya mtoto ni pamoja na ukatili unahusisha matumizi ya nguvu na vitisho kwa mtoto vinavyofanywa na mtu au kikundi cha watu na kusasbisha mtoto kupata madhara ya kimwili na kiafya , ukatili wa kisaikilojia au kingono pamoja na utelekezwaji wa mtoto bila kupata haki zake za msingi .
Ili kuondokana na ukatili huo dhidi ya mtoto nchini,Miho ameto wito kwa wanajamii kutoa taarifa kwa vyombo husika pindi wanapoona kuna kiashirio cha ukatili wa mtoto au kupiga simu namba ya msaada 116 bila malipo.
Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na UNICEF yanayofanyika kwa siku tano ,yanalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mtoto ngazi ya Manispaa kufahamu masuala mbalimbali yanayohusiana na ulinzi na usalama wa mtoto katika kujenga ustawi wa mtoto wa sasa na baadae .
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.