Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Col.Patrick Sawala amewataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kuzingatia kanuni bora za Afya katika kipindi hiki cha msimu wa mvua za masika ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko hususani kipindupindu.
Hayo ameyasema Januari 07,2025 alipotembelea Manispaa ya Mtwara-Mikindani akikagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua na kuongea na wananchi waliopata athari za mvua hizo.
Aidha ametoa wito kwa wananchi kuendelea na moyo wa dhati katika kujaliana kwa kuwahifadhi wenzao waliopata athari za mvua kwa kukosa makazi.
Vilevile amewataka wananchi kuwa watulivu katika kipindi hiki wakati Serikali ikiendelea kujipanga namna ya kuboresha miundombinu ya barabara kwa haraka huku akisisitiza jamii kushiriki kwa nafasi yao ili ziweze kupitika.
Kwa upande wake Yusufu Namanoro mkazi wa Kiyangu B ameiomba Serikali kuboresha Miundombinu ikiwemo ujenzi wa mifereji mikubwa itakayoelekeza maji kwenda Baharini.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara-Mikindani Mhe.Shadida Ndile amesema kuwa Halmashauri inaendelea kufanyia kazi changamoto ya uharubifu WA Barabara Kwa kushirikiana na TARURA.
Manispaa Mtwara-Mikindani
Anuani ya Posta: P. o. Box 92,
Simu ya mezani: 023-2333102
Simu ya mkononi:
Barua pepe: md@mtwaramikindanimc.go.tz
Copyright ©2018Mtwara Mikindani Manispaa . All rights reserved.